Leicester City wameambulia sare ya goli sare ya 1-1 dhidi ya klabu ya Manchester United katika dimba la Old Trafford huku wakitegemea matokeo ya mchezo kati ya Chelsea dhidi ya Tottenham utakaopigwa leo hii majira ya saa nne usiku katika dimba la Stamford Bridge.
kwa matokeo hayo Leicester wanaendelea kubaki kileleni mwa ligi ya England wakiwa na point 77.
Matokeo mengine Liverpool walikiona cha mtema kuni baada ya kuchapwa 3-1 walipokuwa wageni wa Swansea huku Man city wakiambulia kichapo cha mbwa mwizi 4-2 walipowatembelea Sauthampton.


Post a Comment