Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: WAAMUZI KUTOKA GHANA KUCHEZESHA YANGA NA ESPERANCA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mwamuzi Joseph Odartei Lamptey, Jumamosi Mei 7, 2016 anatarajiwa kuwa mwamzi wa kati katika mchezo wa kimataifa kuwania Kombe la Shirikis...
Mwamuzi Joseph Odartei Lamptey, Jumamosi Mei 7, 2016 anatarajiwa kuwa mwamzi wa kati katika mchezo wa kimataifa kuwania Kombe la Shirikisho Barani Afrika utakaozikutanisha timu za Young Africans ya Dar es Salaam, Tanzania na GD Sagrada Esperanca ya Angola.
Lamptey kutoka jiji la Accra, Ghana atasaidiwa na raia wenzake wa nchi hiyo kuchezesha mchezo huo Na. 99. Mwamuzi Msaidizi Na. 1 (line 1) ni David Laryea wakati Mwamuzi Msaidizi Na. 2 (line 2) ni Malik Alidu Salifu.
Mwamuzi Msaidizi mezani (Fourth Official) ni Cecil Amately Fleischer huku Kamishna wa mchezo huo, akiwa ni Asfaw Luleseged Begashaw wa Ethiopia.
Viingilio na upatikanaji wa tiketi utatangazwa kesho Ijumaa Mei 6, 2016 na uongozi wa klabu ya Young African mara baada ya mkutano kati ya makocha wa timu zote mbili. Mkutano wa makocha hao utafanyika saa 5.00 mchana kwenye Ukumbi wa mikutano wa TFF.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top