Bado masaa machache tu kufungwa kwa dirisha la usajili barani ulaya,vilabu mbalimbali barani humo vimeendelea kupigana vikumbo vikiwania saini za wachezaji kutoka klabu fulani.
Mpaka sasa klabu ya Manchester City imefanikiwa kuwatoa wachezaji wake watatu kwenda kwa mkopo katika klabu tofauti tofauti ambao walikuwa hawapo katika mipango ya Pep Guardiola.
Wachezaji waliotolewa na klabu ya Manchester City ni hawa:
• WILFRED BONY
Muivory cost huyu amefanikiwa kupata timu ambayo itamwezesha kuendelea kukipiga katika ligi ya England,Wilfred Bony amesajiliwa kwa mkopo wa muda mrefu na klabu ya Stoke City.
•SAMIR NASRI
Klabu ya nchini Hispania Sevilla Fc imefanikiwa kumsajili mchezaji Samir Nasri kwa mkataba wa mkopo wa muda mrefu akitokea Manchester City.
•ELIAQUIM MANGALA
Eliaquim Mangala amefanikiwa kupata timu na hii kutokana na klabu ya Valencia kumtoa mchezaji wao Mustafi aliye jiunga na Arsenal, Mangala amejiunga na Valencia kwa mkataba wa mkopo wa muda mrefu akitokea Manchester City.


Post a Comment