Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: MAJI MAJI YAANGUKIA PUA UHURU
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea kwa michezo 5 kupigwa katika viwanja mbalimbali Tanzania, kwa upande wa Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu...

Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea kwa michezo 5 kupigwa katika viwanja mbalimbali Tanzania, kwa upande wa Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu klabu ya Dar es Salaam Young Africans walishuka uwanja wa Uhuru Dar es Salaam kuwakaribisha Majimaji FC, hiyo ni baada ya kutoka suluhu na Ndanda FC katika uwanja wa Nangwanda.

Katika mchezo huo wa tatu wa Ligi Kuu kwa Yanga wakiwa wameshinda mchezo mmoja dhidi ya African Lyon na kutoka suluhu na Ndanda FC, umemalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa goli 3-0, magoli ambayo yalifungwa na Deus Kaseke dakika ya 19 na Amissi Tambwe aliyefunga magoli mawili dakika 75 na 85 na kuendeleza rekodi yake dhidi ya Majimaji FC.

Kama utakuwa unakumbuka mchezo wa mwisho wa Majimaji kucheza na Yanga Dar es Salaam January 21 2016 walikubali kipigo cha goli 5-0, huku Amissi Tambwe akipiga hat-trick lakini katika mchezo wa leo Tambwe ameishia kuzinyanyasa beki za Majimaji na kufunga magoli mawili pekee.

MATOKEO MENGINE YA LIGI KUU VODACOM LEO JUMAMOSI TAR 10/09/2016

VODACOM TZ BARA

MWADUI-SHINYANGA
Mwadui 2 Vs Stand 2

SOKOINE-MBEYA
Mbeya City 1 Vs Azam 2

NANGWANDA-MTWARA
Ndanda 0 Vs Kagera 0

MABATINI-PWANI
Ruvu Shooting 1 Vs Jkt Ruvu 0

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top