Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: TATHIMINI: ''SUPER SUNDAY'' NI POCHETTINO DHIDI YA PEP GUARDIOLA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na: Ayoub Hinjo Pep Guardiola alifanikiwa kuondoka na alama zote tatu katika uwanja wa Old Trafford dhidi ya Manchester United ambayo Mour...


Na: Ayoub Hinjo

Pep Guardiola alifanikiwa kuondoka na alama zote tatu katika uwanja wa Old Trafford dhidi ya Manchester United ambayo Mourinho inaonekana alijilaumu kushindwa kutoa nafasi kwa wachezaji ambao walifanikiwa kubadili mchezo kipindi cha pili.

Safari hii Pep Guardiola anaingia White Hart Lane ambako Manchester City alishindwa kuondoka na alama hata moja msimu ulioisha. Hadi sasa Pep Guardiola ana ushindi wa asilimia 100 katika mechi sita za ligi akiwa na alama 18.

Tottenham ni timu ambayo imesukwa kwa miaka mitatu na Maurice Pochettino. Tangu kuingia kwa kocha huyo tayari wameshajua watembee kwa mtindo upi ili kufikia wanachokitaka. Ni timu ambayo inaonekana kuwa na muunganiko kuanzia nyuma hadi mbele.

TOTTENHAM

Miaka 51 imepita tangu Tottenham waanze ligi kwa ubora huu. Hadi sasa hawajafungwa mchezo wowote. Kitu muhimu kwao ni kuwa sasa wanaweza kupata alama muhimu hata kama hawachezi vizuri sababu katika kikosi chao sasa wana watu ambao wanaweza kukupa matokeo.

Mpira wanaocheza Tottenham ni wa kasi na mara nyingi wamekuwa wakitumia pande za pembeni katika kutengeneza mashambulizi ya timu hiyo. Pia wapo vizuri eneo la katikati ambako wamejaa wachezaji ambao wanaweza kuamua matokeo muda wowote. Pia Spurs ni moja ya timu ambazo wanatumia vizuri mipira ya ''set pieces''.

Son Heung-min anaonyesha kuwa Tottenham hawaathiriki kwa kukosekana kwa majeruhi Harry Kane sababu katika michezo mitatu ya ligi kuu England amefanikiwa kufunga magoli manne. Wachezaji wengine pia wanaonyesha ubora wao na hiko ndicho kinachoonekana kuleta maendelea kwa Spurs ya Pochettino.

Pamoja wamekuwa na kitu kinachofanana kama timu katika kufanya majukumu ya timu kwa pamoja. Spurs ni timu ambayo inaonekana kuwa na ulinzi imara hadi sasa wameruhusu magoli matatu katika michezo sita.

MANCHESTER CITY

Pep Guardiola ameonyesha kufanikiwa kiasi katika kutengeneza mpira wa Manchester City na jinsi walivyoanza ligi inaonyesha kuwa watafika level ambayo Pep Guardiola anahitaji.

Manchester City ndio timu ambayo inaongoza katika umiliki wa mpira wakiwa na asilimia 64 za umiliki huo ligi kuu England. Ubora wao mkubwa upo katika kushusha "tempo" ya timu pinzani ili kuweza kumiliki mchezo kiujumla.

Kama Tottenham watakuwa katika tempo ya juu katika kushambulia wanatakiwa kuwa makini na Claudio Bravo ambaye anaonekana kuwa mzuri katika kuanzisha mashambulizi ya kushtukiza kutokea nyuma.

Kupitia Sterling,Nolito,Silva na Aguero kwa pamoja wataonyesha kuwa hawaathiriki na pengo la Kevin De Bruyne ambaye ni majeruhi. Shughuli ya mwisho kwa Pep na timu yake ni kuhakikisha nafasi zinatengenezwa na zinatumiwa vizuri na jicho lao lipo kwa Kun Aguero ambaye yupo juu kwa magoli matano.

Katika mechi sita pekee Manchester City wamefanikiwa kuweka "clean sheet" moja tu. Ni wazi inaonyesha bado Manchester City wanajenga timu yao na kwa aina ya wachezaji wa Tottenham wanaoongoza safu ya ushambuliaji wanatakiwa kuwa makini zaidi.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top