Ligi Kuu soka Tanzania bara iliendelea leo Septemba 25 2016 kwa Mabingwa watetezi wa Ligi hiyo klabu ya Dar es Salaam Young Africans kushuka katika uwanja wa CCM Kambarage kucheza na wenyeji wao Stand United katika mchezo wao wa 5 wa Ligi KuuTanzania bara msimu wa 2015/2016.
Kwa upande wa Stand United waliingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kutoruhusu kufungwa katika michezo yao mitano kabla ya kucheza mchezo wao wa 6 dhidi ya Yanga , wakati Yanga waliingia katika uwanja huo wakiwa na rekodiya kutofungwa mchezo hata mmoja, huku wakiwa wameruhusu sare 1 dhidi yaNdanda FC pekee katika michezo yao mitano.
Katika mchezo huo ambao Stand Unitedwalikuwa wanadhaniwa kama dhaifu dhidi ya bingwa mtetezi Yanga, wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa naPastory Athanas dakika ya 62 na kuifanya ikae nafasi ya pili katika msimamo wa VPL kwa kufikisha point 12 na Yanga kuwa nafasi ya 3 wakiwa na point 10.


Post a Comment