Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: HANS VAN PLUIJM AREJEA KAZINI LEO ASUBUHI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Ilikuwa asubuhi ya furaha kwa kikosi cha Yanga SC pamoja na benchi zima la ufundi mara baada ya kurejea kipenzi chao kazini kocha mkuu Hans ...

Ilikuwa asubuhi ya furaha kwa kikosi cha Yanga SC pamoja na benchi zima la ufundi mara baada ya kurejea kipenzi chao kazini kocha mkuu Hans Van Pluijm katika mazoezi ya timu hiyo leo.

" hamjambo..." alitoa salamu hiyo katika lugha ya kiswahili akionesha ishara ya kuwaita wachezaji wote wamsogelee na kuanza kusali kisha  akatoa risala fupi kabla ya kuanza mazoezi kujiandaa na mchezo wa kesho dhidi ya Mbao FC .

" nawapenda sana na hakika nina furaha sana kuwa nanyi tena baada ya uongozi kuweka mambo sawa. Kikubwa sasa ni kujipanga vyema kushinda michezo yetu yote minne iliyobaki katika mzunguko huu wa kwanza wa ligi.."

"nawaomba sana wanangu tupambane na turejeshe ubingwa wetu kwa mara ya tatu mfululizo kwani ndio nia yetu sisi kama tumu"

"kama ilivyo tamaduni yetu kwetu kila mchezo ni kama fainali nadhani hiki ni kitu ambacho kinajulikana kwa wote"

Pluijm aliongea maneno mengi kwa muda mchache kikubwa kuwapa nasaha wachezaji kujituma muda wote ili kutetea ubingwa wanaoushikilia.

Hakuacha kumshukuru kocha msaidizi Juma Mwambusi kuiongoza vyema timu hiyo kunyakua ushindi wa 4-0 dhidi ya JKT Ruvu wakati yeye akiwa hayupo katika benchi hilo la ufundi baada ya kujiudhuru.

Hans Van Pluijm ametengua uamuzi wake wa kujiuzulu kuifundisha klabu hiyo baada ya kuombwa na uongozi wa klabu pamoja na mwanachama mwandamizi mheshimiwa Mwigulu Nchemba waziri wa mambo ya ndani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hans Van Pluijm ametamba kuzipasua mbao za watoto wa Ilemela toka jijini Mwanza katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara hapo kesho

" tumefurahi kurudi kwa mwalimu maana tumemzoea pia ni rafiki wa wote na mbinu zake tunazielewa vyema kikubwa na mapambano na kuhakikisha ubingwa unabakia jangwani kwani hilo ndio la msingi kwa timu yetu"
alizungumza nahodha wa timu Haruna Niyonzima baada ya mazoezi.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top