Wengi walitazamia sita asimame Kamusoko na Nane Kamusoko kama ilivyokuwa kwa Toto na Kagera lakini wakubwa kila mchezo una tactical and technical approach yake.
Thabani ni natural holding midfielder mwenye uwezo mkubwa kusimama kama kiungo mchezeshaji na mshambuliaji pia lakini uwezo wa kukaba humfanya mwalimu kumsimamisha kama defensive midfielder lakini akitembea na box zote mbili za juu na chini . Na mara nyingi akipangwa hivi lazima awepo kiungo mkabaji namba mbili as back up to him anapotembea na hizo box kama box to box midfielder. ( Kaseke hutumika katika hili)
Sasa kwanini mwalimu leo kaamua kumuanzishia nje?! na kumuacha Haruna peke yake?!
Kama mliwatizama vizuri Mbao FC wakicheza na Simba SC , wanatumia 4-5-1 na hapo kati kuna viungi wakabaji watatu wenye uwezo wa kukata muunganiko wa timu pinzani toka nyuma kuja mbele " direct play" .
Walifanikiwa kuuvunja ufalme wa Simba kwenye kiungo na kuanza kushambulia kwa counter au kutengeneza set pieces ingawa priority ni defence. Omog alibadili plans zake na kuwamaliza jioni sana.
Kwa uchezaji wa Haruna na Kamusoko ambao by 60 % ni wazuri kwenye offensive patterns ukiwaanzisha kwenye timu inayotumia mfumo huu unaweza kujikuta unaua kiungo na timu muda wote kuchezeshwa na wing backs kwa kushambulia kwa upande . Aidha droo au mfungwe wakiweza kutumiq vyema counter zao.
Twite sawa si mzuri kupanda lakini anaweza kupambana pale kati na viungo wawili kama deep lying holding midfilder akipeleka mipira mbele aidha kuitawanya kulia au kushoto ( tactical switching ) au kushirikiana vyema na Kaseke kulia ambae atakuwa anaingia na kutoka .
Changomoto ipo kwa Obrey Chirwa si mzuri kutengeneza daraja na viungo wa kati kama afanyavyo Donald Ngoma ambaye hushuka chini kuweka link up na central midfielders .
Niyonzima atatakiwa kuwa makini sana kuleta muunganiko hapa kati .
Kikosi cha Yanga SC leo dhidi ya Mbao FC
1. Deogratius Munishi
2. Hassani Kessy
3. Mwinyi Haji
4. Andrew Vicent
5. Vicent Bossou
6. Mbuyu Twite
7. Simon Msuva
8. Haruna Niyonzima
9. Amisi Tambwe
10. Obrey Chirwa
11. Deusi Kaseke
Akiba
- Beno Kakolanya
- Pato Ngonyani
- Oscar Joshua
- Thabani Kamusoko
- Juma Mahadhi
- Donald Ngoma
- Mateo Antony
Post a Comment