Kile kiluchokuwa kinasubiriwa kwa hamu kubwa na wana Yanga wengi kwenye kuelekea mabadiliko ya mfumo wa klabu yao si kingine bali ni mkutano mkuu.
Mkutano mkuu ulitarajiwa kufanyika hapo kesho tar 23 kwenye uwanja wa kaunda pale yalipo makoa makuu ya klabu hiyo bingwa mara 26.
Kwenye hali yakushangaza na leo hii mwenyekiti wa Yanga Sc Yusuph Manji aliitisha mkutano na waandishi wa habari majira ya saa sita mchana.
Mwenyekiti akiongea na waandishi kwenye mkutano huo alisema kuwa jana usiku majira ya saa moja alipokea "stop order" ya kusimamisha mkutano mkuu wa wanachama uliokuwa ufanyike kesho hapo kaunda
"baada ya kupokea ilinidi tufanye jitihada za kwenda kwenye vyombo husika na kujiridhisha juu ya usimamishwaji huo kama ni wakweli"
"kama ilivyo lazma tufuate sheria za nchi ni kweli lile simamisho limetoka mahakamani na hatuna budi kufuata kilichoagizwa ila na wahasa wana Yanga msijali kwani tutapeleka vielelezo vyote na tunaamini mtapata haki yanu kama wanachama kufanya maamuzi kidemokrasia kama katiba ya Yanga inavyosema"
Pia mwenyekiti aliongeza kuwa "nawaomba sana radhi wote mlioanza safari na mliokuwa tayari mmefika kwaajili ya mkutano mkuu kesho hautokuwepo pia nawaomba sana msifike hapa kesho tusijeonekana tumekiuka sheria za nchi"
"walionipa kura ni wanachama wa yanga tena kwa imani kubwa na wao ndio wenye maamuzi juu ya maendeleo na mabadiliko katika klabu yao"
"naipenda sana yanga na nipo na yanga mpaka mwisho wala msiwe na wasiwasi wana Yanga wenzangu"


Post a Comment