Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: MOURINHO NDANI YA PEPO YENYE MATESO MAKALI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na: Ayoub Hinjo Ni nani asiyemfahamu Jose Mourinho!? Nadhani hakuna,kuanzia watoto wadogo,wakina mama na hata wazee ambao si wafuasi wa mp...

Na: Ayoub Hinjo

Ni nani asiyemfahamu Jose Mourinho!? Nadhani hakuna,kuanzia watoto wadogo,wakina mama na hata wazee ambao si wafuasi wa mpira wanamfahamu kocha huyo mwenye maneno mengi na mafanikio katika timu alizopita.

Jaribu kuangalia aina ya wachezaji wa Mourinho kuanzia FC Porto,Chelsea,Inter Milan na hata Real Madrid kisha angalia aina ya wachezaji wa Manchester United jinsi walivyokuwa tofauti.

Mbinu ni kitu pekee ambacho Mourinho  amekuwa nacho kwa muda mwingi na kitu kikubwa kwake amezoeleka katika mbinu za uzuiaji "Parking Bus" na kushambulia kwa kushtukiza. Mbinu hii imempa umaarufu zaidi na mara nyingi alifanikiwa kupata alichohitaji.

Mourinho wa Manchester United amekuwa tofauti. Utofauti wake umeanzia kwenye wachezaji ambao amekutana nao pale Carrington. Asilimia kubwa ni wachezaji ambao hawafanani rangi kama wanavyosema ndege wanaofanana huruka pamoja.

Ile siku Mourinho aliyosaini mkataba wa kuitumikia Manchester United alikuwa ameingia kwenye ndoa na mashabiki zaidi ya Milioni 500 duniani kama takwimu zinavyosema. Kumridhisha kila mmoja si kazi rahisi.

Ndoa hiyo ilikuwa ngumu kwa Moyes mwishowe mkataba ukavunjika. Mdachi mwenye heshima zake aliishindwa ndoa hiyo na sasa ni miezi michache tu kwa Jose inaonekana kuwa ngumu.

Mourinho kawa muwazi juu ya hili kuwa hajawahi kufundisha timu inayomiliki mpira kama Manchester United,anapenda jinsi timu yake inavyocheza lakini matokeo yamekuwa hayapatikani,ni jambo ambalo linamuumiza kweli kweli Mreno huyo.

Hazina ya wachezaji ambao yuko nayo ni tofauti kuingiza falsafa zake. Katika michezo mingi ambayo United imekuwa ikiongoza amekuwa na akili ya kuua mchezo "kill game" kwa kufanya mabadiliko ya kuingiza wachezaji wanaozuia. Ni jambo ambalo limeshindwa kumpa faida katika timu hiyo.

Mbinu za Jose kwa United ni kama sumaku mbili zilizoshindwa kuvutana sababu ni pande mbili zinazofanana,na mara nyingi zimekuwa zikikwepana. Naamini kichwa cha Jose hakijajua kuwa kukaa na mpira ni mbinu ya kujizuia pia hasa kutokana na wachezaji ambao kila asubuhi yupo nao Carrington.

Njia pekee ya Mourinho kupata matokeo ni kuifanya timu yake ifunge magoli zaidi kama ilivyo kwa nafasi zinazotengenezwa. Pia kitu cha utofauti kwa Jose ni kukosa kikosi kamili cha kwanza ambacho atakitumia kupata matokeo. Amekuwa akibadili kikosi karibu kila mechi tofauti na wapinzani(Chelsea,Arsenal,Liverpool,Tottenham) wake wa kubwa ambao wameshapata mseto kamili kwenye timu zao.

Mara kadhaa Jose aliitaka kazi ya kuifundisha Manchester United kama timu yake ya ndoto. Ndoto yake imetimia lakini mateso anayokutana nayo katika pepo aliyotaka kuishi ni makali kwake. Muda bado upo kwa Jose Mourinho  kuitengeneza United kuwa pepo anayoitaka lakini kwa mateso haya ni kipimo tosha kwake kuwa United ni timu ya daraja la juu zaidi yenye presha.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top