Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: OLD TRAFFORD: MANCHESTER UNITED vs TOTTENHAM
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
MANCHESTER UNITED Miaka kadhaa nyuma ilikuwa rahisi kutabiri mechi ya Manchester United dhidi ya Tottenham inayofanyika Old Trafford. Laki...

MANCHESTER UNITED

Miaka kadhaa nyuma ilikuwa rahisi kutabiri mechi ya Manchester United dhidi ya Tottenham inayofanyika Old Trafford. Lakini sasa imekuwa sio tena ni kutokana na Spurs kuwa katika daraja lingine la juu tofauti na zamani.

Ushindi dhidi ya Spurs utakuwa ni ufunguo kwa Manchester United katika kupunguza pengo la alama na hasa katika kupambana kwenye nafasi ya kutafuta nafasi nne za juu.

Matokeo katika uwanja wa Old Trafford hivi karibuni yamekuwa magumu kupatikana. Michezo minne ya mwisho iliyopigwa uwanjani hapo matokeo yalikuwa sare.

United wamekuwa wakicheza vizuri katika michezo ya hivi karibuni. Wanatengeneza nafasi,wanamiliki mpira lakini magoli yamekuwa hayafungwi ya kutosha. Kazi kubwa kwao ni kubadilisha matokeo ya sare kuwa ushindi kwao.

TOTTENHAM

Kama tunawaangalia Spurs jinsi wanavyojipanga, mabeki wa pembeni wanatumika kama ufunguo katika kuisukuma timu kwenda mbele.

Wakina Eriksen,Ali na Son wamekuwa wakitengeneza nafasi kwa mabeki wa pembeni kwa wao kuingia ndani ambapo mabeki wa pembeni wa timu pinzani wanakuwa wakiwafuata na kuacha maeneo yao wazi.

Spurs ni moja ya timu ambazo zina uwezo mkubwa wa kujenga mashambulizi kutokea nyuma iwe kwa kupiga pasi fupi au ndefu.

Faida kubwa ambayo Spurs wanayo ni uwezo wa timu yao kupata magoli kwa njia za aina zote kama mipira iliyokufa na hata mpira wa kushambulia kwa kushtukiza.

BATTLE KEY

Upande wa timu zote mbili kuna wachezaji wenye vipaji na uwezo mkubwa katika kuzisaidia timu zao kupata matokeo lakini timu zote mbili uwiano unajengwa na watu wawili ambao ni Carrick na Wanyama.

Carrick amekuwa muhimu sana katika kikosi cha United. Kwenye michezo ambayo amecheza United haijapoteza mchezo wowote. Carrick ni mchezaji wa aina tofauti anayeifamya United iwe na uwiano tofauti na alivyokuwa hapewi nafasi.

Uwepo wa Carrick umesaidia Zlatan kupata mipira mingi akiwa kwenye eneo lake la ushambuliaji tofauti na ilivyokuwa awali ambapo wale watatu walionyuma yake iliwalazimu kushuka chini zaidi kufuata mipira.

Wanyama ni nguzi muhimu kwa Spurs hasa katika kufanya ulinzi kwa mabeki walionyuma yake na hata wale wa pembeni ambao wana kazi ya kusaidia mashambulizi.

Amekuwa na umuhimu zaidi katika kuzuia mipira ya kushtukiza kutoka kwa wapinzani kwa kusimama katika eneo la katikati ambalo linampa uhuru wa kuziba nafasi ambazo mabeki wa pembeni wameziacha na hicho kimekuwa kikimfanya mara nyingi atengeneze utatu na mabeki wa kati Katika kuzuia.

Na: Ayoub Hinjo

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top