Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: TATHIMINI YANGA DHIDI YA JAMHURI SC
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na Samuel Samuel Yanga SC imetupa karata yake ya kwanza kwa kishindo katika mechi yao ya kwanza dhidi ya Jamhuri SC katika michuano ya komb...

Na Samuel Samuel

Yanga SC imetupa karata yake ya kwanza kwa kishindo katika mechi yao ya kwanza dhidi ya Jamhuri SC katika michuano ya kombe la Mapinduzi. Yanga iliifumua Jamhuri goli 6-0.

Ilikuwa ni mechi ya upande mmoja kwa dakika zote 90. Yanga walifanikiwa kuitawala Jamhuri idara zote kwa mbinu na mfumo waliokuwa wakiutumia.

Tuzitazame timu zote katika falsafa za waalimu, mbinu na mifumo iliyotumika.

Jamhuri SC
Kocha wa Jamhuri katika dakika 25 za awali alifanikiwa sana katika mbinu zake za kuwakataa Yanga SC kucheza kwa uwazi ( open game ). Viungo na walinzi wa Jamhuri walikuwa na kazi ya kuufinya uwanja katika mfumo wao wa 4-5-1 . Huu ulikuwa ni mfumo wa kujilinda wakijaza viungo wengi kati na kutumia wings kushambulia hususani wing ya kushoto.

Walifanikiwa kufanya majaribio mawili hatari huku wakiwachanganya Kelvin Yondani na Andrew Vicent kwa kasi , rafu na mchezo wa kukamia hali iliyoleta kutoelewana.

Kosa walilolifanya Jamhuri nikuamini wameweza kuwabana Yanga katika dakika 15 mpaka 20 za kwanza na kubadili mfumo kutoka 4-5-1 na kuingia 4-4-2 wakifunguka na kushambulia kwa kasi bila muhimili mzuri wa kiungo.

Justin Zullu akicheza kama kiungo mkabaji aliwavunja Jamhuri kati kwa kuwapanga viungo wenzake kwenye kiungo cha pembe tatu " triangular midfield ". Yeye na Kamusoko wakisimama sambamba chini huku Haruna Niyonzima aliyekuwa akicheza " free role " akisimama juu yao. Hii iliwafanya wao kulitawala dimba na kuamua mchezo uchezwe vipi. Mifumo ya ulinzi ikisimamiwa na Zullu huku Kamusoko akiwa " driving force kupeleka mashambulizi mbele pia kucheza kama kiungo mshambuliaji kificho. Niyonzima akizunguka kama box to box midfielder. Hapa utaona 4-4-2 ya Jamhuri ilizimww na 4-3-3 ya Yanga SC ingawa wakati mwingine walikuwa 3-5-2 kuwatumia Mwinyi Haji na Juma Abdul kuongeza idadi kati na kutengeneza mashambulizi ya upande.

Mbinu hizi zilizima ndoto za Jamhuri kuibuka washindi katika mchezo huo pia wakajikuta hawana tena muunganikoo kitimu toka nyuma hadi mbele nakuwa watumwa wa kuutafuta mpira.

Yanga SC
Nilipokiona kikosi nilijiuliza nia na madhumuni ya kocha George ni nini katika mechi hii?! kwa ubobezi yoyote yule wa masuala ya kimbinu na kiufundi lazima alijua nini kitawakuta Jamhuri kwa aina ya wachezaji aliowachagua.

Mahesabu ya George ni ya mbali sana ukifanikiwa kuichungulia " notebook " yake. Iwe ligi kuu au michuano hii ya Mapinduzi, yeye anachotazama ni maandalizi yake ya michuano ya klabu bingwa Afrika.

Yanga SC haijamleta kwa ajili ya FA , ligi kuu au kombe la Mapinduzi bali kufika mbali michuano ya klabu bingwa Afrika.

Akitazama kulia na kushoto kwake anawaona Mwambusi na Hans Van Pluijm hawa wote wameitendea Yanga makubwa katika vikombe hivyo lakini sio klabu bingwa Afrika. Hili linamfanya kukuna kichwa usiku na mchana kufikia rekodi mpya ndani ya klabu hiyo.

Malengo hayo ndio yalimfanya kuingiza kikosi cha maangamizi uwanjani na akiwataka wachezaji wake kucheza kwa kufuata maagizo yake , kujituma muda wote na kuonesha uwezo mkubwa kama wapo mbele ya Al Ahly , Zanaco au APR.

Yanga waliingia kwa mfumo wa 4-3-3 wakitumia walinzi wanne nyuma ; Abdul , Haji , Andrew na Yondani . Viungo watatu juu ; Zullu, Kamusoko na Niyonzima huku Msuwa akimaliza juu kulia , Emanuel Martin juu kushoto na Ngoma akisimama kati kama target man.

Ushindi wa goli sita za Yanga hakika unaanzia kwenye safu ya viungo wa chini waliokuwa wamejipanga vyema na kusambaza mipira kwa akili sana . Hii iliwachukua dakika 43 tu! kutengeneza goli nne.

Zullu akijipanga vyema kati na wenzake katika mfumo wa triangular waliweza kufanya switching kulia kwa Msuva na kushoto kwa Martin aliyekuwa mwiba mzuri kwa kasi na krosi zake pia Zullu akipiga pasi murua ndefu za kati kuleta muunganiko wa haraka na forward line.

Heko kwa Msuva dakika ya 19 akifungua kalamu ya magoli lakini pia akitengeneza goli mbili kwa wenzake.

Kimbinu Yanga SC imekuwa na uwezo mzuri wa kumiliki mpira , kupiga pasi za uhakika na kushambulia kwa kasi pembe zote.

Lwandamina kafanikiwa kurudisha fighting spirit kwa kila mchezaji ndani ya timu . Juma Makapu anaonekana kuimudu vyema nafasi ya kiungo mkabaji na jana ameongeza kitu cha ziada . Anakaba kwa akili , amejaribu pasi nne ndefu kwenda mbele , akipunguza pasi za nyuma na rafu zisizo na maana hii inaonesha faida yakuwa na " matured  player " ndani ya timu kwenye nafasi yako na kumtizama ili ujifunze zaidi . Technically hii ni positive impact ya kumtazama Zullu na kumsikiliza kocha wake.

Bado tatizo kwa Mwashuiya . Licha yakupewa nafasi na mwalimu lakini mabadiliko si makubwa kwake kiuchezaji . Mbinu pekee anayoijua ni mbio na kupita krosi . Upigaji wake hauna malengo kama ilivyo kwa Emanuel Martin . Yamfaa kujichunguza zaidi nafasi yake ndani ya timu hiyo kwa ujio wa Martin pia Deusi Kaseke.

Mara nyingi kombinesheni ya  Yondani na Dante huwa si imara sana kwa ulinzi wa kati . Wote ni "sweepers " hii hujikuta wanashindwa kujua nani awe mtu wa kwanza kupokea mpira wa kwanza na yupi amzunguke mwenzake au kumfanyia masking golikipa . Wote wanatabia ya kupanda juu au kutanuka pembeni ndio maana Hans wote alikuwa anawajenga kumzunguka Nadir au Bossou; hawa ni walinzi viongozi . Lakini jana nimeona mabadiliko makubwa kwa Dante akicheza vyema nafasi ya ulinzi kumzunguka Yondani . Muda mwingi yeye ndio alikuwa akifanya clearance na kuhakikisha haondoki nyuma mpaka mstari wa marking upo salama.

Naiona Yanga yenye mabadiliko makubwa kiuchezaji kwa mbinu na mifumo yake . Tuzidi kuwatizama michezo ijayo.

Wapinzani watambue Yanga haijaja Zanzibar kujaribu kikosi au kuwapumzisha wachezaji wake wa kikosi cha kwanza bali wapo mazoezini kwa malengo ya klabu bingwa mapema mwezi ujao hivyo wajipanga kwa upinzani mkali.

Asanteni.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top