Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: YANGA HII SASA SIFA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Michuano ya Kombe la Mapinduzi 2017 imeendelea katika uwanja wa Amaan. Leo hii ilipigwa  michezo ya Kundi B  kwa mara ya kwanza, mchezo wa ...

Michuano ya Kombe la Mapinduzi 2017 imeendelea katika uwanja wa Amaan.
Leo hii ilipigwa  michezo ya Kundi B  kwa mara ya kwanza, mchezo wa Kwanza ukiwa ni Azam dhidi ya Zima moto saa 10 jioni wakati Yanga wakicheza dhidi ya Jamhuri ya Pemba katika mchezo uliochezwa saa 2.15 usiku.

Yanga ambao walishusha kikosi chao kamili, walifanikiwa kuifunga Jamhuri ya Pemba goli 6-0, idadi ambayo imewafanya kuwa ndio timu ya kwanza katika michuano ya Kombe la Mapinduzi 2017 kufungwa idadi kubwa ya magoli katika mchezo mmoja.

Magoli ya Yanga yalifungwa na Simon Msuva dakika ya 19, 40, Donald Ngoma dakika ya 23, 37, Thabani Kamusoko dakika ya 59 na goli la mwisho la Yanga lilifungwa na Juma Mahadhi akitokea benchi, kwa matokeo hayo Yanga wanapata nafasi ya kuongoza Kundi B wakiwa na point 3 sawa na Azam FC ila Yanga anaongoza kwa tofauti ya goli 5.

Katika mchezo huo kiungo toka Zambia Justine Zulu ambae alianza kwenye kikosi cha kwanza kwa mara ya kwanza tangu ajiunge ma klabu ya Yanga Sc aliumia na kupelekea kushonwa nyuzi nne juu ya jicho baada ya kugongana na mchezaji wa Jamhuri na kushindwa kuendelea na mchezo baada ya kipindi cha pili kuanza.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top