Mabingwa Afrika timu ya Mamenlody sundowns wameawasili nchini Tanzania jana kwa ziara maalumu ya kampeni ya kuzuia mauaji ya Tembo.
Ujio wa mabingwa hawa wa Afrika hapa nchini ilikuwa ni pamoja na kupata nafasi ya kucheza na vilabu viwili wikubwa hapa nchini Yanga na Simba ikiwa ni moja ya maandalizi yao kuelekea mchezo wao dhidi ya Tp Mazembe toka Congo.
Kwa upande wa vilabu vya Simba na Yanga wote wameshindwa kucheza mechi dhidi ya mabingwa hao kwa kila mmoja kubanwa na ratiba za ligi Tanzania bara . Yanga wakijiandaa jumamosi jumapili dhidi ya Stendi United na Simba SC dhidi ya Majimaji jumamosi ugenini.
Mashabiki wengi na watu wengi wa soka wamekuwa wakilalamika juu ya hilo ila kwa upande wangu n naamini wenye mtazamo wa jicho la tatu kisoka na pia wanaotambua kujitambua kwa timu wataunga mkono kuwa Yanga na simba wapo sahihi kwenye kushindwa kucheza na Mabingwa hao wa Afrika.
Embu tujiulize swali moja Je Yanga au simba wangeenda Afrika ya kusini wakati ligi kuu ina endelea je wangepata nafasi ya kucheza na Mamenlodi?
Kwa upande wangu naamini ingekuwa ngumu sana labda wangepewa timu B ya mabingwa hao wacheze nao tena Asubuhi kipindi wanapofanya mazoezi yao. Hili limewagi kuwakuta Azam FC walipozulu nchini Afrika Kusini.
Mimi nawapa sifa kubwa sana Simba na Yanga kwenye kuonyesha ukomavu juu ya kuheshimu ratiba zao na kutambua wapo kwenye kipindi gani kwa sasa.
Sidhani kama simba au Yanga kama wanauhitaji wowote wa mechi ya kujipima nguvu wakati wapo kwenye ligi tena kipindi ambacho ligi imechanganya na inaushindani mkubwa sana.
Mabingwa wa Afrika watusamehe tuu kuwakosa Simba na Yanga kwani kwa upande wangu wako sahihi kabisa juu ya ukataaji wao kwenye hili.
Haya ni Mawazo na Mtazamo wangu Mimi naamini kila mmmoja ana mtazamo wa fofauti juu ya hili.
Lakini hii iwe changamoto kwa waandaaji wa ziara hii . Walitakiwa kuzipa taarifa mapema timu hizi au kutumia muda ambao hawabanwi na ratiba kwa mipango hii mizuri kwa ujirani mwema na kuleta changamoto chanya kimbinu.
Mamelodi na waandaaji wasiitafsiri hii ni dharau bali ni mgongano wa ratiba tu .
Godlisten anderson Chicharito.
@zechicharito
Post a Comment