Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: CITY KATIKA HATIHATI YA KUMKOSA JESUS MSIMU MZIMA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Imeripotiwa kuwa mshambuliaji wa Man City Gabriel Jesus anaweza kuwa nje ya uwanja kwa kipindi chote cha msimu kilichobaki kufuatia kuumia k...

Imeripotiwa kuwa mshambuliaji wa Man City Gabriel Jesus anaweza kuwa nje ya uwanja kwa kipindi chote cha msimu kilichobaki kufuatia kuumia katika mguu wake kwenye mechi ya jana dhidi ya Bournemouth ambayo City walishinda goli 2-0.

Jesus ambaye ametua City mwezi Januari akitokea Palmeiras kwa ada ya pauni milioni 27, leo ameonekana akiwa amavaa kiatu cha kujikinga (Protective Boot) huku akitembea kwa msaada wa magongo huko jijini Manchester.

Taarifa kutoka kwa klabu ya Man City inathibitisha kuwa Mbrazil huyo amevunjika mfupa (The Fifth Metatasar) katika mguu wake wa kulia na atapata vipimo zaidi siku zijazo ili kujua ni kwa muda gani atakaa nje.

Gabriel Jesus mpaka sasa ameichezea City mechi 5 akifunga jumla ya magoli matatu.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top