Klabu bingwa Tanzania bara Yanga Sc leo hii inatupa karata yake ya kwanza kwenye michuano ya klabu bingwa Africa dhidi ya timi ya Ngaya ya uko Moroni Comoro.
Mchezo unatarajiwa kuanza saa tisa kamili kwa saa za comoro ikiwa ni sawa na saa nane na dk 57 kwa saa za Tanzania kwenye uwanja wa Estade de Bommel wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 5000 tu.
Baada ya Donald Ngoma kuendelea kuuguza majeraha yake naona mwalimu George atakuwa hana wasiwasi kwani Obrey Chirwa kwa sasa yupo kwenye kiwango kizuri na ameweza kufanya kile anacho agizwa na mwalimu.
Kikosi cha mabingwa hao kitakachoanza leo hii ni kama
1. Deogratius Munishi
2. Juma Abdul
3. Mwinyi Haji
4. Nadir Haroub
5. Kelvin Yondani
6. Justin Zullu
7. Saimoni Msuva
8. Thabani Kamusoko
9. Amisi Tambwe
10. Obrey Chirwa
11. Haruna Niyonzima
Akiba
- Ali Mustafa
- Hassani Kessy
- Oscar Joshua
- Emanuel Martin
- Juma Mahadhi
- Juma Saidi
- Deusi Kaseke


Post a Comment