Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: WAYNE SHAW AAMUA KUJIUZULU
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kipa wa Klabu ya Sutton United Wayne Shaw inayoshiriki National League nchini England amefanya maamuzi ya kujiuzulu kutokana na tukio lake l...

Kipa wa Klabu ya Sutton United Wayne Shaw inayoshiriki National League nchini England amefanya maamuzi ya kujiuzulu kutokana na tukio lake la kula la Uwanjani kwenye mechi ya juzi dhidi ya Arsenal.
Maamuzi haya ameyafanya baada ya tume ya Ubashiri na FA kuanza kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo.
Kocha Mkuu wa Sutton United Paul Doswell amethibitisha kuwepo na makubaliano baina ya kipa  huyo na Klabu mara baada ya Chama  Cha Mpira wa Miguu nchini England FA na tume ya ubashiri kuthibitisha kuanza kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo lililosambaa mitandaoni kumuonesha Shaw akiwa anakula huku mchezo ukiwa unaendelea.

Kampuni ya Ubashiri ya Sun Bets(Wadhamini wa jezi wa Sutton United) kabla ya mechi iliweka odds za 8-1 kuwa kipa huyo angeweza kula uwanjani wakati mchezo unaendelea.
Shaw 46, ambaye alikua kipa wa akiba katika Mchezo huo wa FA Raundi ya tano alionekana akiwa anakula katika benchi la timu ya Sutton wakati mchezo unaendelea ambapo walipoteza 2-0.

Hivyo uchunguzi unaendelea ili kujua kama kipa huyo alihusika katika upangaji wa ubashiri huo ambapo ni uvunjaji wa sheria za ubashiri na adhabu itamkuta endapo atakutwa na hatia.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top