Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: AZAM TV KWA HILI SIWAUNGI MKONO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kampuni ya kurusha matangazo ya luninga yavAzam media ambayo hurusha moja kwa moja michezo ya ligi kuu Tanzania Bara leo hii wameam...



Kampuni ya kurusha matangazo ya luninga yavAzam media ambayo hurusha moja kwa moja michezo ya ligi kuu Tanzania Bara leo hii wameamka na kuitaka bodi ya ligi kusogeza muda wa mechi za ligi hiyo kutoka kuchezwa saa kumi na kusogezwa nyuma mpaka saa 9 alasiri.

Ni mechi mbili tu zimechezwa mpaka sasa kwa kila timu tangu kuanza kwa ligi kuu Tanzania bara wadhamini hao wenza wa ligi hiyo kubwa kabisa nchini Tanzania ambao wana miliki katika urushaji wa matangazo ya luninga wamefikia hatua hiyo baada ya kituo hicho kupata mkataba wa kuonyesha ligi kuu ya nchini Spain alimaaruufu kama Laliga.

Hii itawapa fursa ya kuonyesha ligi hiyo iliyosheheni wanasoka bora wa dunia.

Hata hivyo Vilabu vikubwa nchini Tanzania Simba na Yanga tayari vimekataa ombi hilo kwa kusema halina mashiko kwani ni ngumu sana kumwambia shabiki aje uwanjani saa nane kuja kutazama mechi tena katikati ya wiki wakati muda huo bado unakuwa ni muda wa kazi kwa hapa nchini kwetu.

Vilabu hivyo vikongwe na vyenye mashabiki wengi wamesema wao wako tayari hata kujitoa kwenye mkataba wao na Azam media kuliko kukubaliana na hayo matakwa wanayo yataka Azam media.

 USHAURI WANGU
Ingekua ni Bora Azam media iongeze channel za tv zao ili waweze kukidhi mahitaji ya wateja wao na pia waangalie wajue kuwa hapa ni Tanzania na itakua kosa kubwa sana kuwapa nafasi Laliga kuliko ligi kuu ya bara pamoja na kwamba mimi sifahamu mkataba kati ya Azam na laliga wala Azam na bodi ya ligi
TFF muwe makini sana juu ya hili pamoja na mikataba ya aina hii kwani kiukweli inafanya TFF ichafuke taswira yake juu ya mikataba ambayo wanaingia na wadhamini wao.

Simba na Yanga ambao mechi zao nyingi ndizo zinazorushwa moja kwa moja kujitoa kwao itaturudisha nyuma hatua mia wakati huu ambapo Tunashuhudia ligi ikizidi kuimarika na hii itatuvuruga sana na sidhani kama itaijenga Azam media.

 Azam media tunawapenda sana kwa mnachokifanya hapa Tanzania ila kwa hili mmmh mmepepesa.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top