Baada ya kupigwa X-Rays madaktari waligundua kwamba Beki
wa Man United,Luke Shaw ameweza kuvunjika mfupa wake Mara mbili pindi
alipochezewa rafu mbaya na mchezaji wa Psv Eindhoven Moreno katika
mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Alipata jeraha hili katika mguu wake wa kulia na usiku ule ule wa
Jumanne aliweza kufanikiwa operation ya kwanza ndogo ambayo ilikuwa ya
kunyosha mfupa ambao ulisogea,baada ya hapo Juzi jioni uongozi ulikaa na
madaktari waka shauri kwamba Shaw lazima afanyiwe operation ya kuunga
mfupa haraka iwezekanavyo.
Luke Shaw atafanyiwa operation ya pili siku ya leo
Ijumaa katika mji wa Eindhoven na baada ya hapo anatarajia kurujea
Nyumbani,Manchester siku ya Jumamosi ya wiki hii.
SIO VIBAYA KUFANYA MAOMBI KWAAJILI YAKE,UGUA POLE KIJANA WETU MUNGU YUPO PAMOJA NA WEWE.
GET WELL SOON LUKE SHAW
Post a Comment