Mshambuliaji wa Yanga aliyetemwa Simba misimu miwili iliyopita Amis Tambwe amesema amefurahi sana kuifunga timu yake ya zamani na anajisikia amani kwa sasa kwasababu wapinzani wao waliongea maneno mengi kabla ya mchezo wao.
Tambwe ameongeza kuwa, wala hakuwa na ‘mchecheto’ na alicheza kawaida kama anavyocheza kwenye mechi nyingine lakini alikuwa na lengo la kuhakikisha anaisaidia timu yake ipate ushindi
“Nafurahi sana sana, tena sana kuifunga Simba, dakika 90 ndio zinaamua uwanjani, mwanasoka huwezi ukasema muda ufike tuwapige unatakiwa kujiandaa kwa kila mechi ili timu yako ishinde, alisema Tambwe.
“Mimi wala sikuwa na presha, nimeshacheza mechi kubwa nyingi kwahiyo kwangu mechi ya leo ilikuwa ya kawaida tu. Kwanza ukicheza kwa presha mpira utakushinda nilikuwa nacheza mpira wangu wa kawaida tu ule ambao huwa nacheza siku zote. Sikuwa nikicheza ili nionekane wala watu waniongelee”.
“Simba walikuwa wanaongea sana kabla ya mchezo wa leo, walisema wametuandalia supu ya mawe na kachumbari ya miba na misumari, basi hiyo supu na kachumbari wakaile wao. Sisi tulibaki kimya tukajiandaa vizuri na leo tumeshinda ndio maana mimi nimefurahi sana”.
Malimi Busungu ni mchezaji mpya kwenye kikosi cha Yanga aliyesajiliwa kwenye dirisha kubwa la usajili akitokea timu ya Mgambo JKT ya jijini Tanga, kwenye mchezo dhidi ya Simba aliingia uwanjani dakika ya 34 kipindi cha kwanza kuchukua nafasi ya Simon Msuva na kutengeneza goli la kwanza kabla hajafunga goli la pili.
Malimi Busungu ni mchezaji mpya kwenye kikosi cha Yanga aliyesajiliwa kwenye dirisha kubwa la usajili akitokea timu ya Mgambo JKT ya jijini Tanga, kwenye mchezo dhidi ya Simba aliingia uwanjani dakika ya 34 kipindi cha kwanza kuchukua nafasi ya Simon Msuva na kutengeneza goli la kwanza kabla hajafunga goli la pili.
Baada ya Busungu kuingia, Yanga ilionekana kubadilika na kuzidi kuwa imara. Mtandao huu uliona ni vyema kuzungumza na Busungungu ili kujua kocha wa Yanga Van Pluijm alimwambia akafanye nini atakapoingia uwanjani kuchukua nafasi ya Msuva.
“Kocha aliniambia nikiingia uwanjani natakiwa niongeze nguvu, na kuhakikisha naubadilisha mchezo kwa kuongeza presha kwa mabeki wa Simba hasa pale tunapokuwa tunawashambulia na kutumia vizuri nafasi yoyote tutakayoipata”, amesema Busungu.
“Nashukuru Mungu nimefunga goli la kwanza dhidi ya Simba nikiwa Yanga goli ambalo limeamua mchezo kwasababu baada ya kuwafunga goli la kwanza, Simba walianza kujipanga na kutengeneza mashambulizi ili wasawazishe lakini nilipofunga goli la pili mipango yao yote ikafa na muda ulikuwa tayari umekweda sana”.
“Mwalimu ndiye anaamua nani aanze na nani asubiri, mimi naheshimu maamuzi ya mwalimu kwasababu yeye ndiye mpangaji wa timu. Na kuanzia nje haimaanishi kwamba mchezaji hana kiwango ila inawezekana ni mipango ya mwalimu kulingana na mechi anayokutana nayo kwahiyo mimi kuwa Yanga na kuanzia nje hainipi presha itafika wakati na mimi nitacheza kwenye kikosi kinachoanza”.



Post a Comment