Mzunguko wa raundi ya sita ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania (VPL)
unatarajiwa kuendelea kesho Jumamosi na Jumapili kwa timu 10 kucheza
kusaka alama 3 muhimu.
Jijini Tanga Mgambo Shooting watakua wenyeji wa Coastal Union katika
uwanja wa Mkwakwani, Majimaji FC watawakaribisha Mwadui FC uwanja wa
Majimaji mjini Songea.
Jumapili Stand United chama la wana watawakaribisha watoza ushuru wa
jiji la Mbeya (Mbeya City) katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga,
huku Kagera Sugar wakiwa wenyeji wa Tanzania Prisons uwanja wa Ali
Hassan Mwinyi mjini Tabora na Toto Africa watakua wenyeji wa JKT Ruvu
jijini Mwanza uwanja wa CCM Kirumba.
VPL KUENDELEA KESHO
Title: VPL KUENDELEA KESHO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mzunguko wa raundi ya sita ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) unatarajiwa kuendelea kesho Jumamosi na Jumapili kwa timu 10 kucheza ku...



Post a Comment