Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: AC MILLAN YAMBURUZA KORTINI YAFFA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
AC Milan imembu ruza mchezaji wake wa zamani mwenye umri wa miaka 19 Yusupha Yaffa mahakamani kwa madai ya udanganyifu kuwa umri wake sa...


AC Milan imembu ruza mchezaji wake wa zamani
mwenye umri wa miaka 19 Yusupha Yaffa
mahakamani kwa madai ya udanganyifu kuwa
umri wake sahihi ni miaka 28

Juma lililopita ilikuwepo makala ya wachezaji
kutoka Afrika wanavyodumaza soka kwa
kudanganya umri , punde si punde limezuka hili,
habari za kusikitisha sana kwa soka la Afrika na
waafrika walioko ughaibuni.

Bila shaka imani za klabu kubwa ya Ulaya kwa
wachezaji wa kiafrika itapungua iwapo matukio
kama haya yataendelea.

Klabu ya AC Milan imeamua kumpandisha
kizimbani mchezaji Yusupha Yaffa raia wa
Gambia kwa madai ya kudanganya umri.
Yaffa aliiambia AC Milan kwamba umri wake ni
miaka 19, lakini baadaye iligundulika wakati
huo alikuwa na umri wa miaka 28.

Licha ya kuwa sasa yuko nchini Ujerumani
akikipiga katika klabu ya MSC Duisburg lakini
bado AC Milan imeshikilia bango kuhusiana na
shauri hilo la kupunguza umri kwa miaka tisa.

Kama ilivyoripotiwa na La Gazetta dello Sport,
mchezaji huyo amesema mara kadhaa kuwa
alipoteza nyaraka zake za utambulisho wakati
akihamia ughaibuni.
Pamoja na kwamba mwanasheria wa Yaffa,
amekuwa akipambana na kukanusha hilo,
marafiki wengi wa Yaffa kutoka Afrika hasa
nchini mwake wamekuwa wakiendelea kupalia
makaa ya moto kutokana na kueleza kupitia
mitandao ya kijamii miaka waliyosoma naye,
kucheza naye soka na wanajua kwamba ni
mkubwa miaka tisa kuliko alivyojieleza.

Suala la wachezaji wa Kiafrika kudanganya umri
limekuwa kubwa sana. Safari hii hata wale
wanaokuja kucheza soka Tanzania pia
wamekuwa wakidanganya umri pia.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top