Huyu ndio mkali wetu wa siku leo ...
Anjulikana kama " bull dowzer" " heavy weight" huyu si mwingine bali ni mshambuliaji wa kati toka nchini Zambia katika mkoa wa Kitwe , Davies Mwape aliyevuma na Young Africans SC msimu wa 2010-11 na 2011-12 .
Mwape ana urefu wa futi 5'7" akijaaliwa umbo kubwa lililokaa misuli imara hali inayompa uwezo wa kupambana na backline yoyote. Simba wanamjua vizuri mtu huyu.
Mwape kama ilivyo kwa magwiji wengi wa soka nchini Zambia alianzia soka lake katika timu ndogo lakini maarufu sana nchini Zambia iliyoko maili chake toka mjini Kitwe inayojulikana kwa jina la Chambishi FC. Hii timu ipo katika mji mdogo wa Chambishi ikikumbukwa sana kuwatoa nyota wa Zambia ndani ya ligi kiu na walioko Ulaya kama marehemu Mosses Chikwalakwala mmoja wa malegendary wa Zambia waliofia kwenye ile ajali ya ndege mwaka 93. Chikwalakwala alikuwa mchezaji tegemeo wa KK 11 akitokea Chambishi FC.
Wakali wengine waliovuma kwa safari zao kuanzia Chambishi timu inayoshiriki first Division ni Webster Chikabala bonge la midfielder wengine ni Zico Chande na Emmanuel Sibawe ambao wapo katika nyoyo za wazambia mpaka leo. Chambishi ni kama Abajalo hapa Tanzania.
Mwape baada ya kuvuma na timu hiyo , wlipata wakala mzuri aliyemtafutia team nchini Afrika kusini katika team ya Orlando Pirates aliyeichezea mechi 8 tu bila kufunga goli lolote. Hakupata mafanikio mazuri na team hii ikumbukwe ndio kwanza alikuwa anaanza soka la kulipwa bila kupitia ligi kuu nchini kwao yaani ni sawa na safari ya Thomas Ulimwengu nchini DRC . Hiyo ilikuwa mwaka 2005-06.
Alitimkia FC AK msimu wa 2006-7 ambako alionesha uwezo mzuri kwa mechi 14 alizocheza akitupia goli 5 ndipo Jomo Cosmos walipomuona na kumpa kandarasi ya miaka miwili 2007-09 lakini kandarasi hiyo haikudumu Mwape hakuonesha kiwango kizuri . Ilichangiwa sana na Injuries hivyo alidumu kwa mwaka mmoja tu 2008 akarudi nyumbani kuchezea Zanaco FC . Aliichezea mechi 22 za ligi akitupia goli 8 lakini napo hakudumu sana baada ya kujiunga nao mwaka 2009 tu , alijiunga na team kongwe katika ligi ya nchi hiyo ya Konkola Blades iliyoanzishwa mwaka 1956 maeneo ya Chilililabombwe.
Akiwa na Konkola Blades ndipo Mwape alipoanza kuonesha uwezo mkubwa wa kusakata kabumbu eneo la ushambuliaji kwa kutupia magoli muhimu na ndipo mabosi wa Yanga SC walipomuona mkongwe huyu na kuingia nae mkataba mwaka 2010 uliodumu hadi mwaka 2012 alipotimkia Roan United iliyopo nchini mwao ambao wanajulikana kama wahuni wa Kafubu.
Kuhama hama team na kukosa mafanikio mazuri mwanzoni kulimfanya Mwape kuichezea mechi chache timu yake ya taifa akicheza mechi 6 tu mwaka 2005-6.
Lakini katika safari yake yote hiyo anayakumbuka sana maisha yake ndani ya Yanga SC hususani upinzani wa jadi kati ya Simba SC na Yanga SC . Goli lake katika Kagame CUP likibaki kumbukumbu nzuri sana moyoni mwake nchini Tanzania .
Kumbukumbu zinaonesha Mwape mwenye umri wa miaka 29 sasa, alisaini mkataba na Zanaco FC mwaka 2013 baada ya kuachana na wahuni wa Kafubu katikati ya mwaka 2012.
Huyo ndio mkali wetu wa siku ndugu yangu.
Imeandaliwa na ;
Samuel Samuel


Post a Comment