Kuna uwezekano kuwa Chelsea ikashuka daraja, amesema kocha wa muda wa klabu hiyo Guus Hiddink. Chelsea wapo katika nafasi ya 14 kwenye msimamo, pointi sita kutoka timu tatu zilizopo mkiani, na mechi zao mbili zijazo ni dhidi ya Everton na Arsenal.
"Ni ukweli uliopo," amesema Hiddink, ambaye alichukua nafasi ya Jose Mourinho mwezi Disemba.
"Tuna mechi mbili ngumu.
"Usipopata pointi katika hizo, hujui timu nyingine zitafanyaje. Ligi Kuu inaweza kukushangaza." ameongeza Hiddink.
Chelsea walikuwa pointi moja juu ya ukanda wa kuteremka daraja, wakati Mourinho alipoondoka.
About Author
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Advertisement

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment