Kocha wa kilabu ya Manchester United Louis Van Gaal amesema kuwa anaamini kilabu yake bado ina nafasi ya kushinda ligi ya Uingereza.’
Mshetani wekundu’ baada ya kuishinda Liverpool 1-0 katika uwanja wa Anfield siku ya jumapili na kusogea hadi nafasi ya tano katika msimamo wa ligi hiyo,wakiwa pointi saba pekee nyuma ya viongozi wa ligi hiyo Arsenal na Leicester ilio nafasi ya pili.
”Kuna mechi nyingi ambazo zimesalia”,alisema Van Gaal alipoulizwa iwapo timu yake itapigania taji hilo.
”Ni lazima tuendelee”,ijapokuwa si rahisi,lakini tunaweza kufanikiwa kwa sababu tunaonyesha kila wiki kwamba tunaweza”.


Post a Comment