Pele " the black pearl "
Pele " the global icon of football "
Gwiji hili la soka duniani ambaye anashikiria rekodi ya mchezaji bora wa karne ya 20 aliyopewa na FIFA mwaka 1999 ameingia matatani na wadau wa soka la kisasa hasa vijana.
Pele amenukuliwa na mitandao mbalimbali ya habari duniani bado akijisifu na kutoamini hakuna kiumbe ambaye anaweza kuja kuvunja rekodi zake licha ya kasi inayooneshwa na Lionel Messi na Cristian Ronaldo.
Pele mtandao wa Guiness World Records unamtambua kama mfungaji bora mwenye rekodi ya pekee duniani akicheza mechi 1363 na kufunga magoli 1283 katika ligi rasmi na michuano mingine.
Anaongoza kuifungia timu yake ya taifa ya Brazil kwa magoli 77 katika mechi 91 alizoichezea hali iliyomfanya raisi wa Brazil mwaka 1962 kumtangaza kama " lulu ya taifa".
Pele hadi sasa anashikiria rekodi ya kupiga hat trick 92.
Anaheshimika kama most successful Top Division Goal scorer akitupia magoli 541.
Pele ana rekodi ya kijana mdogo kucheza fainali za kombe la dunia 1958 na pia kupiga hat trick katika umri mdogo.
Ikumbukwe gwiji hili ndio mwanzilishi wa tick taka .
Ana mengi mazuri ya kukumbukwa lakini kauli zake za mara kwa mara za kutothamini vipaji vinavyo chipukia kwa kuwapa maneno ya kukatisha tamaa kwamba hakuna wakuja kuvunja records zake kuna mpunguzia sana heshima yake duniani.
Hasimu wake mkubwa duniani Diego Maradona mara kadhaa amekuwa akiwakashifu FIFA kwa upendeleo juu ya Pele na kuwaambia ana amini yeye ni bora kuliko Pele.
Wadau wengi wa soka nyakati za hivi karibuni wamekuwa wakimuona Pele kama mtu muoga kupotezwa katika records za duniani.
Post a Comment