Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: REAL MADRID NA ALTLETICO MADRID ZAFUNGIWA KUSAJILI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Miamba wa Uhispania Real Madrid na Atletico Madrid wamepigwa marufuku kutonunua wachezaji wapya sokoni vipindi viwili. Klabu hizo zimeadhib...

Miamba wa Uhispania Real Madrid na Atletico Madrid wamepigwa marufuku kutonunua wachezaji wapya sokoni vipindi viwili.
Klabu hizo zimeadhibiwa na shirikisho la soka duniani Fifa kwa kukiuka sheria za uhamisho wa wachezaji kuhusu kununuliwa kwa wachezaji ambao bado ni watoto.
Marufuku hiyo haitaathiri kipindi cha sasa cha kununua wachezaji, ambacho kinaendelea hadi mwisho wa mwaka huu.
Atletico pia wametozwa faini franka 900,000 za Uswizi ambazo ni sawa na pauni 622,000 za Uingereza, nao Real wakatakiwa kulipa franka 360,000 (£249,000).

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top