Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: TETESI KUTOKA BARANI ULAYA: VAN GAAL, MESSI, GUARDIOLA, CAVANI, MATIP, KROOS, NEYMAR
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Meneja wa Manchester United Louis van Gaal, 64 anakabiliwa na mchezo mgumu dhidi ya Liverpool siku ya Jumapili, huku uongozi wa klabu hiyo ...

Meneja wa Manchester United Louis van Gaal, 64 anakabiliwa na mchezo mgumu dhidi ya Liverpool siku ya Jumapili, huku uongozi wa klabu hiyo ukiwa na wasiwasi juu ya nafasi ya timu yao kufuzu kwenye Ligi ya Mabingwa. (Chanzo Times)

Wazamini wa Manchester United kampuni ya Adidas wanamtaka mshambuliaji wa Barcelona na Argentina Lionel Messi, 28, aje kuungana tena na Pep Guardiola, ambaye ataondoka Bayern Munich mwishoni mwa msimu, akija Old Trafford. (Chanzo Marca)

Meneja wa Paris St-German Laurent Blanc amesema tabia za mshambuliaji wake Edinson Cavani zimekua ni tatizo na atamuachia mchezaji huyo wa kimataifa wa Uruguay mwenye umri wa miaka 28 aondoke. (Chanzo Daiky Mail)

Chelsea wametoa ofa ya paundi millioni 40 kwa kiungo wa Real Madrid Mjerumani mwenye umri wa miaka 26 Toni Kroos, ambaye amehususishwa pia na Liverpool pamoja na Manchester United. (Chanzo Fichajes, kupitia Daily Star)

The Blues wanashindana na Inter Milan na Barcelona kwenye kumuwania mshambuliaji wa Paris St-German Ezequiel Lavezzi, 30. (Chanzo Daily Mirror)

Liverpool wamekubali kumchukua mlinzi wa kati wa Schalke, Mcameroon Joel Matip, 24, kwa ada ya bure mwishoni mwa msimu. (Chanzo Daily Mirror)

Mkurugenzi wa Bayern Munich Matthias Sammer bado hajaweka wazi kama kiungo Mjerumani Mario Gotze mwenye umri wa miaka 23, ambaye inaaminika kuhitajiwa na klabu ya Liverpool, ataendelea kubakia na mabingwa hao wa Ujerumani au la. (Chanzo Daily Express)

Manchester United wanakalibia kumsajili beki wa kati mwenye umri wa miaka 24 kutoka nchini Austria Aleksandar Dragovic anayekipiga Dynamo Kiev kwa ada ya paundi millioni 16. (Chanzo Sport Mediaset, kupitia Daily Express)

Mshambuliaji wa West Brom Saido Berahino, 22, anaweza akaendela kubaki kwenye klabu hiyo kwa kipindi chote cha msimu kilichobakia kutokana na Tottenham kutokua tayari kulipa tena paundi millioni 23 waliyokuwa wanataka kulipa kipindi kilichopita, huku bosi wa Spurs Pochettino akiwa hana uhakika kama Berahino ni mshambuliaji sahihi anayemuhitaji. (Chanzo Sun)

Stoke wanata kumchukua Berahino – na wanaamini watawashinda Tottenham kwenye kumsajili mchezaji huyo anayekipiga Under-21 kwenye timu ya taifa ya Uingereza. (Chano Times)

Mshambuliaji wa West Ham Andy Carroll, 27, anaweza akawa nje ya uwanja kwa miezi miwili kutokana na tatizo la misuli. (Chanzo Daily Mail)

Mshambuliaji wa Charlton Ademola Lookman anahitajiwa na Manchester City pamoja na Chelsea, huku Everton na Tottenham wakionyesha pia nia ya kumuhitaji mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18. (Chanzo Independent)

Beki wa kushoto wa Chelsea Mghana Baba Rahman, 21, anazidi kuchanganyikiwa kutokana na kukosi nafasi kwenye kikosi cha kwanza tangu alipojiunga na the Blues akitokea Augsburg mwezi Agosti. (Chanzo Bild, kupitia Guardian)

Mshambuliaji wa Barcelona Neymar, 23, ameamuliwa kutokea mahakamani juu ya usajili wake wa kwenda Nou Camp akitokea klabu ya Santos ya nchini Brazil mwaka 2013. (Chanzo Guardian)

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top