Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: VARDY NJE WIKI MBILI BAADA YA KUPASULIWA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mshambuliaji nyota wa Leicester City Jamie Vardy hataweza kucheza kwa wiki mbili baada yake kufanyiwa upasuaji. Fowadi huyo wa Uingereza am...

Mshambuliaji nyota wa Leicester City Jamie Vardy hataweza kucheza kwa wiki mbili baada yake kufanyiwa upasuaji.
Fowadi huyo wa Uingereza amefanyiwa upasuaji mdogo kwenye mtoki wake, kituo cha redio cha BBC cha Leicester kimeripoti.
Vardy amekuwa matata sana msimu huu na mabao yake 15 aliyoyafunga Ligi ya Premia yamesaidia Bweha hao kupanda hadi nambari mbili ligini.
Mchezaji huyo wa umri wa miaka 28 amechezea klabu hiyo mechi 24 msimu huu.
Vardy alicheza kwenye kikosi cha mkufunzi Roy Hodgson cha Uingereza kilichofuzu kwa michuano ya Euro 2016.
Alichezea klabu yake dakika zote 95 mechi dhidi ya Bournemouth ambayo walitoka sare ya 0-0 Jumamosi.
Kabla ya kujiunga na Leicester, Vardy alichezea klabu ya Fleetwood Town.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top