Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: MTANZANIA MISHETTO AENDA KUFANYA MAJARIBIO CZECH
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mtanzania Charles Mishetto ameondoka Ujerumani na kwenda kufanya majaribio katika klabu moja nchini Jamhuri ya Czech. Taarifa za uhakika zi...

Mtanzania Charles Mishetto ameondoka Ujerumani na kwenda kufanya majaribio katika klabu moja nchini Jamhuri ya Czech.

Taarifa za uhakika zimeeleza, Mishetto aliyekuwa anaichezea Rabestein FC inayoshiriki Ligi Daraja la Nne nchini Ujerumani sasa yuko Jamhuri ya Czech.

“Kweli Mishetto yuko Czech anafanya majaribio, ninajua ni timu ya daraja la pili, ila sijajua ni timu gani. Iwapo atafanikiwa au kutofanikiwa nitakutaarifu,” kilieleza chanzo kutoka Ujerumani.

Rabestein FC inashiriki Ligi Daraja la Nne nchini Ujerumani na Mishetto alikuwa mmoja wa wachezaji tegemeo.

Mishetto amewahi kukipiga Stand United ya mjini Shinyanga kabla ya kuanza kupambana kutafuta maisha ya soka barani Ulaya.

Juhudi za kumpata Mishetto mwenyewe aweze kufafanya hilo bado zinaendelea

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top