Timu ya Taifa ya Wanawake ya Mpira wa Miguu “Twiga Stars” inatarajiwa
kusafiri siku ya Ijumaa kuelekea nchini Zimbabwe kwa ajili ya mchezo
wake wa marudiano wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa
Wanawake zitakazofanyika mwishoni mwa mwaka huu nchini Cameroon.
Kikosi cha Twiga Stars kinaendelea na mazoezi katika uwanja wa Karume
chini ya kocha mkuu, Nasra Juma kujiandaa na mchezo huo muhimu ili
kuweza kusonga mbele katika hatua inayofuata.
Kuhusu maendeleo ya kambi, kocha Nasra Juma amesema vijana wake
wanaendela vizuri, wamekua wakiendelea na mazoezi tangu baada ya mchezo
wa awali na ana imani watafanya vizuri katika mchezo wa marudiano.
Twiga Stars inahitaji ushindi katika mchezo huo wa marudiano
utakaochezwa Jumapili, Machi 20 katika uwanja wa Rufalo uliopo jijini
Harare ili kuweza kufuzu kwa hatua ya pili ya michuano hiyo.
TWIGA STARS KUWAFATA ZIMBWABWE IJUMAA
Title: TWIGA STARS KUWAFATA ZIMBWABWE IJUMAA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Timu ya Taifa ya Wanawake ya Mpira wa Miguu “Twiga Stars” inatarajiwa kusafiri siku ya Ijumaa kuelekea nchini Zimbabwe kwa ajili ya mchez...



Post a Comment