Kaimu Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), Martin Chacha amejiuzulu nafasi yake katika utumishi wa
TFF kuanzia leo tarehe 5 Aprili 2016.
Katika barua yake aliyomwandikia Katibu Mkuu wa TFF, Chacha alieleza
kuwa amepata majukumu mapya ya kikazi ambayo pamoja na majukumu ya
kifamilia yatamfanya akose muda wa kutumika vema katika nafasi yake
katika Shirikisho
Martin alijiunga na TFF Julai 2014 akiwa Afisa wa Mashindano na
baadaye kuteuliwa kukaimu nafasi ya Mkurugenzi wa Mashindano, kufuatia
aliyekuwa anashikiria nafasi hiyo Boniface Wambura kuteuliwa kuwa
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB).
TFF inamtakia kila la kheri na mafanikio mema Chacha katika majukumu yake mapya.
CHACHA AJIUZULU TFF
Title: CHACHA AJIUZULU TFF
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kaimu Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Martin Chacha amejiuzulu nafasi yake katika utumishi wa TFF...



Post a Comment