TIMU ya Taifa ya Vijana wa chini ya Miaka 17 ya Tanzania, maarufu kama Serengeti
Boys, Leo imewafunga wenzao wa Egypt waitwao The Pharaohs Bao 3-2
katika Mechi ya Kirafiki iliyochezwa huko Azam Complex, Chamazi, kwenye
Viunga vya Jiji la Dar ess Salaam
Hii ni mara ya pili kwa Timu hizi kupambana na katika Mchezo wa awali uliochezwa
Jumamosi katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam, Serengeti Boys
waliibuka na ushindi wa mabao 2 – 1 dhidi ya The Pharaos huku Mabao ya
Serengeti yakifungwa na Cyprian Bennedictor na Ally Hussein.
Serengeti Boys wapo chini ya Makocha Bakari Shime na Sebastian Mkomwa wakishauriwa na Kocha kutoka Denmark Kim Paulsen.
Michezo
hii ya kirafiki ni sehemu ya maaandalizi kwa Timu zote mbili
zinazojiandaa na kufuzu kucheza Fainali za Mataifa Afrika kwa Vijana
mwaka 2017 zitakazofanyika nchini Madagascar.
Kwenye
Mashindano hayo katika Mechi za Mchujo Serengeti Boys itaivaa
Shelisheli hapo Juni 25, 2016 katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es
salaam na marudiano kuchezwa baada ya Wiki moja nchini Shelisheli.
Hii
Leo huko Azam Complex, The Pharaohs walitangulia kufunga kwa Bao la
Dakika ya 22 la Mostafa Elyas na Serengeti kusawazisha Dakika ya 27
Ibrahim Abdallah na kisha Boko Seleman akaipigia Bao la Pili na la 3 kwa
Serengeti kufungwa Dakika ya 60 na Ibrahim Abdallah.
The Pharaohs walipata Bao lao la Pili Dakika ya 74 Mfungaji akiwa Diaa Wahid na Mechi kwisha kwa ushindi wa Tanzania wa 3-2.
VIKOSI:
Serengeti Boys:
Kibwili, Kibwana, Kibabige, Hussein, Issa, Ngazi, Cyprian, Zubeir, Ibrahim, Boko, Asad
The Pharaohs:
Shobir, Elyas, Hassan, Atef, Tarek, Tolba, Shawer, Gabr, Osama, Mohamed, Saad
SERENGETI BOYS YATISHA
Title: SERENGETI BOYS YATISHA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
TIMU ya Taifa ya Vijana wa chini ya Miaka 17 ya Tanzania, maarufu kama Serengeti Boys, Leo imewafunga wenzao wa Egypt waitwao The Pharaohs ...



Post a Comment