Mshambuliaji wa Uingereza Jamie Vardy
atakosa mchezo wa ligi kuu kati ya Leicester City dhidi ya Manchester United
Jumapili baada ya kuongezewa adhabu kutokana na utovu wa nidhamu.
Vardy alimkaripia mwamuzi wa mechi
Jon Moss baada yake kuoneshwa kadi nyekundi wakati wa mechi yao dhidi ya West
Ham tarehe 17 Aprili ambayo iliisha sare ya 2-2.
Baada ya kukosa mechi ya Jumapili
ambayo Leicester walishinda 4-0 dhidi ya Swansea, Vardy sasa pia atakosa mechi
hiyo ya jumapili.
Mchezaji huyo wa miaka 29 pia
amepigwa faini ya £10,000.



Post a Comment