Liverpool imefanikiwa kuingia hatua ya fainali ya ligi ya Ueropa baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Villarreal.
Wakiwa nyuma kwa bao moja katika mchezo wa awali, Liverpool walisawazisha matokeo baada ya Bruno Soriano kujifunga. Daniel Sturridge aliongeza bao la pili baadaye na kuanza kuidididmiza timu hiyo kutoka Uhispania baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Roberto Firmino.
Adam Lallana alipigilia msumari wa mwisho kwa kufunga bao la tatu usiku wa Alhamisi na kufanya mambo kuwa 3-0.
Kwa matokeo hayo watakutana katika fainali na mabingwa watetezi Sevilla mjini Basel Mei 18
Sevilla walifika fainali kwa kuwacharaza Shakhtar Donetsk kwa matokeo ya jumla ya 5-3.







Post a Comment