Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imetangaza
Uchaguzi Mkuu wa Klabu ya Yanga kuwa utafanyika Juni 25, 2016 badala ya
Juni 5, 2016.
Kamati ya Uchaguzi ya TFF imelazimika kufanya hivyo kwa kuzingatia ushiriki wa Yanga ambayo inashiriki michuano ya kimataifa.
Sekretarieti ya Yanga ambayo ingefanya kazi kwa pamoja na Kamati ya
Uchaguzi kwa kushirikiana na TFF kwa sasa inashughulikia pia kuiandaa
timu kwa ajili ya michuano ya kimataifa.
Yanga inatarajiwa kucheza na Esperanca ya Angola katika michuano ya
Kombe la Shirikisho Barani Afrika Mei 7, mwaka huu kabla ya kurudiana
kati ya Mei 17 na 18, mwaka huu huko Angola.
Kwa mujibu wa ratiba mpya, fomu za kuwania uongozi wa Yanga zitaanza
kuchukuliwa Mei 25, 2016 na kwamba uchaguzi huo utafanyika ndani ya muda
ambao Serikali kwa kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) iliagiza
uchaguzi kufanyika kabla ya Juni 26, 2016 hivyo uchaguzi utafanyika
ndani ya wakati.
Katiba itakayotumika ni ya mwaka 2010 na kwamba Wanachama wa Yanga watatumia kadi za kawaida za uanachama na si za benki.
UCHAGUZI YANGA WASOGEZWA MBELE, SASA JUNI 25
Title: UCHAGUZI YANGA WASOGEZWA MBELE, SASA JUNI 25
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imetangaza Uchaguzi Mkuu wa Klabu ya Yanga kuwa utafanyika Juni 25, 2016 badala y...



Post a Comment