Katika kuelekea kufungua msimu mpya wa ligi kuu nchini Uingereza,kocha wa Arsenal Arsene Wenger amefunguka kuwa matumizi ya pesa yaliyofanywa na Man United si kigezo pekee kuwa watapata ubingwa wa ligi hiyo.
Wenger ataanza ligi jumapili hii akiwakaribisha Liverpool Emirates Stadium,lakini ameendelea kushangazwa na matumizi makubwa ya man united katika usajili.
Mfaransa huyo amesema kutumia zaidi ya pauni milioni 150 katika usajili haihakikishi kuwa Man United watarudi kileleni mwa ligi hiyo.
.
"Man United ni klabu tajiri duniani, si kila timu italeta ushindani katika kiasi cha pesa,lakini haileti tofauti kwa sababu tunaweza kushindana uwanjani na hicho ndio cha muhimu, hatushindani pesa,ni soka" amesema Wenger.
.
"Ushindani wa pesa hauna maana sana katika mbio za ubingwa, watizame Leicester Msimu uliopita" aliongeza
Post a Comment