Rais wa TFF, Jamal Malinzi amepokea kwa masikitiko kifo cha Boniventur Munishi ambaye ni Baba mzazi wa Golikipa wa Young Africans na timu ya Tanzania 'Taifa Stars' , Deogratius Munishi.
Kifo cha Munishi kilitokea jana Agosti 28, 2016 jijini Dar es Salaam.
Kutokana na kifo hicho, Rais Malinzi ametuma salaam za rambirambi kwa familia na ukoo wote wa Munishi akiwasii kuwa watulivu wakati huu mgumu kwao kwa kumpoteza mpendwa wao.
Mungu aipumzishe Roho ya Marehemu mahali pema peponi.
Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.
IMETOLEWA NA TFF


Post a Comment