Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: WENGER AZUNGUMZIA USAJILI WA POGBA MAN U
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Leo Katika uzinduzi wa msimu mpya wa ligi kuu nchini Uingereza, kocha wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa kiungo Paul Pogba atawa...

Leo Katika uzinduzi wa msimu mpya wa ligi kuu nchini Uingereza, kocha wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa kiungo Paul Pogba atawafaa Manchester United.

Pogba,23, amejiunga na mashetani hao akitokea Juventus kwa ada ya Pauni milioni 89 ambayo inaweza kuongezeka zaidi kutokana na vipengele vilivyowekwa.
.
"Thamani ya Mchezaji inategemea na kipaji chake, matarajio ya uimara wake katika timu,umri wake na bei yake ya mauzo" amesema Wenger. "Unapomzungumzia Pogba, hivyo vyote kwake viko sawa, lakini tupo katika mfumo ambao ni mgumu kueleweka. Inabidi tufuate bei zinazolipwa na watu wengine. Na bei zimepanda kwa sababu ya upatikanaji wa pesa umekuwa mkubwa, ndio maana tunaweza kuzidi Pauni milioni 100 kwa mara ya kwanza" amesema kocha huyo.

Pia kocha huyo amesema kuwa rekodi ya dunia ya uhamisho ya Pogba imesababishwa hali ya soko la usajili la sasa ambapo timu za Uingereza zinalazimishwa kulipa zaidi katika manunuzi kuliko timu za mataifa mengine.
.
"Kama utaenda Hispania na wewe ni klabu ya Uingereza, utakuta mfumuko wa bei. Katika klabu za Ufaransa,wao kwa wao , bei za kawaida lakini kama timu ya Uingereza ukienda , bei inapandishwa sana kwa sababu wanajua England kuna pesa". Amesema Mfaransa huyo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top