Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: ARGENTINA BADO BORA DUNIANI KISOKA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Shirikisho la soka duniani FIFA wametoa oradha ya viwango vya soka ulimwenguni katika mwezi huu wa Septemba,Hapo awali katika orodha iliyoto...

Shirikisho la soka duniani FIFA wametoa oradha ya viwango vya soka ulimwenguni katika mwezi huu wa Septemba,Hapo awali katika orodha iliyotoka mwezi August ilituonyesha kwamba Argentina bado akishikilia nafasi ya kwanza na ndivyo anavyo endelea mpaka sasa katika mwezi huu akiwa bado yupo nafasi ileile.

Taifa la Brazil wameweza kusogea katika nafasi moja juu kutoka nafasi ya 5 mpaka sasa kuwa nafasi ya 4. Colombia nao wameporomoka katika nafasi mbili chini kutoka nafasi ya 2 mpaka sasa kuwa nafasi ya 5.

Taifa la Ujerumani limepanda nafasi moja juu kutoka nafasi ya 4 hadi kuwa ya 3,Taifa la Uingereza na Hispania wao wameondolewa katika 10 bora na kushushwa chini Hispania wakishika nafasi ya 11 na Uingereza nafasi ya 12.

Ukija katika bara la Afrika bado Ivory Coast na Algeria wanaonyeshana ubabe kwa kupishana nafasi moja,mwezi uliopita Algeria alikuwa nafasi ya 34 lakini sasa ameshushwa na Ivory Coast kwa nafasi moja hivyo basi Ivory Coast wapo nafasi ya 34 na Algeria 35.

Ukija katika ukanda wetu wa Afrika Mashariki bado Uganda anatuongoza kwa kushika nafasi ya 65 akifuatia Kenya mwenye nafasi ya 91, Tanzania inazidi kupotea katika viwango hivi kwa kushuka takribani viwango vinane kutoka katika nafasi ya 124 mwezi uliopita mpaka nafasi ya 132 mwezi huu.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top