Michuano ya Ligi ya Mabingwa ulaya katika msimu huu inaonekana ni msimu ambao kutafungwa idadi ya magoli mengi zaidi kuliko misimu yote iliyopita. Juzi Jumanne katika michezo Saba yalifungwa magoli 20 na usiku wa jana yaani Jumatano katika michezo 9 yamefungwa magoli 28.
Klabu ya Manchester City baada ya mchezo wao kuhairishwa siku ya Jumanne usiku wa Jana Jumatano waliweza kuwazibua klabu ya Ujerumani Borrusia Monchengladbach goli 4-0,Magoli matatu yalifungwa na Sergio Aguero na Moja lilifungwa na Iheanacho.
Vile vile mabingwa wa Ligi kuu ya England klabu ya Leicester City ilifanikiwa kuanza vyema katika michuano hii ya Uefa wakiwa ugenini kwa kuwafunga Club Brugge magoli 3-0,magoli yaliyo fungwa na Marc Albrighton na Riyad Mahrez aliyefunga mara mbili.
Cristiano Ronaldo na yeye akiwa na Real Madrid katika dimba la Santiago Bernabeu aliweza kufanga bao la 94 katika michuano ya Uefa na kuisaidia klabu yake kupata ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Sporting Cp ya Ureno,goli la pili la Madrid lilifungwa na Alvaro Morata.


Post a Comment