Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: HATIMAE NGASA ATUA JIJINI SALAMA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mrisho Halfan Ngasa ni Mtanzania aliekuwa akicheza soka lakulipwa uko nchini Afrika ya kusini. Alikuwa akicheza kwenye klabu ya Free state ...

Mrisho Halfan Ngasa ni Mtanzania aliekuwa akicheza soka lakulipwa uko nchini Afrika ya kusini.

Alikuwa akicheza kwenye klabu ya Free state ambayo inashiriki ligi kuu ya nchi hiyo ijulikanayo kama PSL

Ni tar 25 mwezi huu Ngasa alivunja mkataba na klabu hiyo ya nchini afrika kusini na kuwa mchezaji huru kucheza popote pale baada ya makubaliano kati yake yeye na klabu yake hiyo kufikia tamati.

Leo hii Ngasa amewasili hapa Tanzania kutoka uko nchini Afrika ya kusini majira ya saa 11 na dk 55 saa za hapa Tanzania.

Baada ya kufika Ngasa alizungumza na blog hii na kusema
"Nikweli mimi na free state tumemalizana kwa amani na sasaivi mimi ni mchezaji huru naweza cheza popote"

"Nafuraha nimefika salama na nimekuja nyumbani kupumzika kidogo ila kuhusu naelekea wapi iyo ipo chini ya meneja wangu mimi siwezi sema lolote"

Mrisho Ngasa ameshawai vichezea vilabu vyote vikubwa vya hapa nchini.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top