Michuano ya kombe la Cecafa kwa wanawake imemalizika leo rasmi kwa timu ya Tanzania Queens kutoka nchini Tanzania kunyakua ubingwa huu huko nchini Uganda.
Timu ya Tanzania ya wanawake (Tanzania Queens) imefanikiwa kutwaa taji hili kwa mara ya kwanza kwa kuanzishwa michuano hii mwaka huu iliyofanyika nchini Uganda. Tanzania Queens wamechukua ubingwa kwa kuwafunga majirani zao timu ya taifa ya wanawake kutoka Kenya.
Timu ya wanawake kutoka Kenya walikubali kupokea kichapo cha magoli 2:1 kutoka kwa Timu ya Tanzania,timu ya Tanzania iliweza kupata magoli 2 ndani ya dakika 45 za kipindi cha kwanza na hapo baadae timu ya Kenya ndio ilipata goli la kufutia machozi katika dakika ya 74.
Magoli mawili ya Tanzania yalifungwa na Mwanahamisi Omary aliyeweza kufunga mara mbili katika mchezo huu.


Post a Comment