Kiungo wa Man City Yaya Toure leo ametangaza rasmi kustaafu kuichezea timu ya Taifa ya Ivory Coast ambayo ameitumikia kwa miaka 14
Toure,33, ameichezea timu hiyo mechi 102 na kufunga goli 19 huku akiwaongoza tembo hao kubeba kombe la mataifa Afrika mwaka 2015
.
"Baada ya kucheza kwa miaka 14 sasa nimeamua kustaafu kuichezea Ivory Coast.
Maamuzi mengine ni magumu kuyachukua lakini ni muda wa kuachia nafasi kwa ajili ya wachezaji wengine.
Ninawashukuru wote walionisapoti na mashabiki zangu." amesema hivyo kiungo huyo.


Post a Comment