Baada ya kupoteza michezo miwili katika ligi kuu ya England na mmoja wa Europa ligi klabu ya Manchester United leo hii imeingia uwanjani kivingine baada ya kuwagaragaza mabingwa wa tetezi wa ligi Leicester City.
Leicester City imepata kipigo cha magoli 4-1 katika dimba la Old Trafford,Man United waliweza kupata magoli 4 katika kipindi chote cha kwanza na kipindi cha pili Leicester City ndio waliweza kurudisha goli dakika ya 60 likifungwa na Dermani Gray
.Manchester United walijipatia magoli 4 yaliyofungwa na Chris Smalling katika dakika ya 22 na dakika ya 37 Juan Mata aliifungia tena,Marcus Rashford aliipatia United goli la tatu katika dakika ya 40 na dakika mbili baadae Paul Pogba aliifungia United goli lake la kwanza tangu ajiunge na klab hii.
Manchester United imefikisha pointi 12 katika michezo 6 ambayo wamecheza mpaka sasa.


Post a Comment