Klabu ya Manchester United imetangaza kuingiza mapato ya Pauni milion 515.3 kwa mwaka wa fedha 2016 na kuwa klabu ya kwanza ya Uingereza kuingiza kiasi hicho.
Katika mwaka huo timu hiyo ilishinda kombe la FA,ilisaini mikataba 14 ya wadhamini na biashara,mapato ya mechi,mapato ya Televisheni yameongezeka
Sasa inakadiriwa mapato hayo kufikia pauni milioni 540 kwa mwaka 2017 licha ya kuwa hawapo katika michuano ya klabu bingwa ulaya.
Man United imekuwa timu ya kwanza ya Uingereza kufikia mapato ya nusu bilioni ndani ya mwaka mmoja, wakiweka rekodi ya faida pauni milioni 68.
Mabingwa wa La Liga Barcelona mapema mwaka huu walitangaza kuingia mapato ya pauni milioni 571, hivyo Man United wamekuwa wapili kwa mapato Barca wakiwa wa kwanza.
About Author
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


Post a Comment