Dereva Fellipe Massa wa timu ya Williams ametangaza kuwa atastaafu mara baada ya msimu huu wa Formular 1 kumalizika.
Mbrazil huyo,35,katika miaka 14 aliyoshiriki katika Formular 1 amewahi kuwa mshindi katika Grand Prix 11 , na hajawahi kuwa bingwa wa mashindano hayo.
Katika msimamo wa Formular 1 msimu huu mkongwe huyo anashika nafasi ya 10 akiwa na pointi 39 huku nafasi ya kwanza ikishikiliwa na Lewis Hamilton mwenye pointi 232 .


Post a Comment