Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: SIMEONE ATHIBITISHA KUPUNGUZA MKATABA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone leo amethibitisha kuwa amepunguza mkataba wake wa kuitumikia timu hiyo. Mkataba wake ambao alisaini ...

Kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone leo amethibitisha kuwa amepunguza mkataba wake wa kuitumikia timu hiyo.

Mkataba wake ambao alisaini machi 2015 ulikuwa umalizike mwaka 2020, baada ya kupunguza miaka miwili, sasa utaisha mwaka 2018.

Simeone ,46,hajaweka wazi kwa nini amefanya hivyo ,lakini amesema pande zote zimefikia makubaliano ambayo ni sahihi.

Muargentina huyo amesema kuwa anafuraha kuwa na Atletico na katika miaka miwili iliyobaki anaweza akasaini mkataba mpya

Simeone ameanza kuifundisha timu hiyo mwishoni mwa mwaka 2011, ameiwezesha kuchukua kombe la La Liga mara moja (2014), kombe la mfalme (2013) na wakiingia fainali ya klabu bingwa ulaya mara 2, zote wakifungwa na Real Madrid.

#ElCholo

Cc ws14

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top