Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: STARS WAVUNA MAPESA PAMOJA NA KUFUNGWA NIGERIA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Pamoja na kipigo Stars wavuta mkwanja Nigeria. Licha ya kupoteza mchezo wa jana dhidi ya Nigeria, Taifa Stars wamevuna kitita cha dola 10,0...

Pamoja na kipigo Stars wavuta mkwanja Nigeria.

Licha ya kupoteza mchezo wa jana dhidi ya Nigeria, Taifa Stars wamevuna kitita cha dola 10,000 kutoka kwa Gavana wa jimbo la Akwa Ibom State, Udom ambapo ndipo unapopatikana Uwanja wa Uyo uliotumika kwenye mchezo wa jana.

Kitita hicho ni sawa na shilingi za Kitanzania ml 21.7 na Gavana huyo alitoa wakati waliokuwa wakipata chakula cha usiku kwa pamoja baada ya mchezo huo.

Ikumbukwe kuwa katika historia ya timu hizi mbili, Tanzania haijawahi kuifunga Nigeria katika michezo yote waliyowahi kukutana zaidi ya kuambulia vichapo na sare.

Gavana huyo ametoa kiasi hicho cha fedha kutokana na ari ya upiganaji iliyooneshwa na wachezaji wa Stars, ambao walikuwa wakiongozwa na nahodha wao Mbwana Samatta ambaye kabla ya mchezo huo alikuwa gumzo kwa Wanigeria.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top