Image and video hosting by TinyPic Image and video hosting by TinyPic
 

Unknown Unknown Author
Title: BADO NI BORA NA NGUZO IMARA YA MAFANIKIO JANGWANI Hans Van Pluijm.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Hans Van Pluijm katika misimu miwili ameweza kuipeleka Yanga SC michuano ya klabu bingwa Afrika na msimu wa mwisho ikiangukia kombe la shir...

Hans Van Pluijm katika misimu miwili ameweza kuipeleka Yanga SC michuano ya klabu bingwa Afrika na msimu wa mwisho ikiangukia kombe la shirikio hatua ya nane bora.

Amweza kuipa klabu klabu hiyo kombe la ligi kuu msimu wa 2015-16 huku yeye mwenyewe akiibuka kocha bora wa ligi . Akicheza mechi 30 katika ligi kuu , sare 7 na kufungwa mechi 1 tu.

Ameweza kuiongoza vyema timu hiyo kunyakua kikombe cha FA ikiwa ni msimu wa kwanza baada ya miaka kadhaa kutofanyika .

Ikumbukwe mafanikio yote hayo kwa msimu uliopita alikuwa na wachezaji 24 tu kwenye kikosi chake . Ambao ukimtoa Tinoco ambaye hakucheza hata mechi moja , aliweza kutumia wachezaji 23 tu kusaka mafaniko ndani na nje.

Mpaka sasa kwenye msimu huu mpya wa ligi 2016-17 Pluijm ameiongoza Yanga kwenye mechi 7 ikishinda mechi 4 , sare 2 na kupoteza mchezo mmoja dhidi ya Stand United.

Pluiijm na benchi lake la ufundi akisaidiana vyema na Juma Mwambusi , wameweza kuendeleza na kutoa nafasi kwa wachezaji wanaoingia kwenye kikosi hicho . Wameweza kumjenga Deusi Kaseke kusimama kama mchezaji tegemeo ndani ya klabu hiyo akitokea Mbeya City.

Malimi Busungu msimu wa 2015-16 akitokea Mgambo JKT alijitahidi sana kumpa nafasi kuonesha ubora wake . Kinda huyo akikumbukwa sana na watani wao wa jadi alipocheza kwa ubora mzuri msimu uliopita yeye na Tambwe wakawaliza Simba 2-0. Majeruhi na masuala mengine hususani nidhamu ya kutunza kipaji yamemtoa mchezaji huyu kwenye njia ya mafanikio ingawa bado waalimu wana tumaini nae.

Mateo Antony katikati ya safu kali ya ushambuliaji ligi kuu Amisi Tambwe na Donald Ngoma lakini Pluijm amekuwa akimpa nafasi mchezaji huyu tokea KMKM ya Zanzibar akitengeneza mbadala mzuri kimbinu kwenye safu ya Ushambuliaji . Kama sio Paul Nonga kuondoka katika klabu hiyo tayari kombinesheni yao ilianza kukubali hususani kwenye mechi ngumu za mikoani au mechi za kukamia.

Ingizo jipya la Andrew Vicent , Juma Mahadhi , Kessy na Beno Kakolanya tayari baadhi yao wameanza kuonekana lulu Jangwani kwa mwalimu huyu kuwapa nafasi huku akiwapumzisha wakongwe.

Ana mengi sana mwalimu huyu yenye faida na kila mwanayanga mwenye jicho jema la kutazama msingi wa mafanikio ya klabu ataona .

Wengi wameanza kushuku uwezo wa mwalimu huyu bila kusimama kwenye misingi ya mbinu , ufundi , falsafa na historia ya timu . Tena wakianza kutumia maneno makali yasiyo na shukrani wala adabu lakini nitoe rai yangu Hans bado ni dira njema ya mafanikio.

Wengi wamekuwa wakisema mwalimu anawabania vijana kucheza kwenye kikosi chake jambo ambalo ukituliza kichwa si kweli .

Jana kocha Mwambusi msaidizi wake amekaririwa na vyombo vya habari akisema wana kawaida ya kubadili kikosi kila baada ya mechi tano ingawa mabadiliko hufanyika wakati wowote pale inapohitajika . Mfano vijana kama Mwashuiya alikuwa nje mwezi mmoja na wili mbili akiunguza jeraha na mara zote akiwa fiti mwalimu alikuwa anawatumia yeye na Msuva kama " super sub " kwenye mipango ya kuongeza kasi ya mchezo.

Makapu Juma ambaye wengi wanampigia upatu kusimama kama suluhisho eneo la kiungo cha chini. Mara kadhaa mwalimu kampa nafasi na si haba kaonesha ubora wake lakini kimbinu hushindwa kubaki katika ubora wake kama kiungo mshambuliaji kutokana kuwa na makosa mengi. Pluijim anatumia mbinu za Total Football zinazohitaji kiungo wa chini kusimama kama chanzo cha ulinzi na ushambuliaji na asicheze kama deep lying holding midfielder ambaye anakabia chini na kufanya sana kazi za ulinzi kuliko kuisukuma timu mbele kimashambulizi . Hali hii humfanya Makapu muda mwingine kutumia nguvu nyingi kwenye blocking hivyo kupata kadi au majeraha ya mara kwa mara. Ndio maana mwalimu humtumia Kamusoko au Twite ambao kwa kiasi kikubwa ni wazuri kwenye nafasi hii ingawa bado kwa asilimia zote.

Mwisho niseme jambo moja , ushawishi wa aina yoyote kumuondoa mzee huyu pasipo kuangalia masuala ya msingi kinacho ikuta Azam FC kitapiga hodi jangwani . Tujifunze kuwa na simile kuwavumilia waalimu pale timu zinapoyumba kidogo.

Samuel Samuel

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top